Swali: Katika chuo kikuu tuna mwalimu anasema kuwa kufanya Tawassul kwa jaha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kitu kimewekwa katika Shari´ah na kwamba kuna upokezi mmoja wa Imaam Ahmad. Vilevile anasema kuwa kuwatukana Maswahabah sio kufuru na khaswa kumtukana Abu Bakr na Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Isitoshe jengine ni kwamba analingania katika uhuru wa dini. Vipi tutaamiliane na mtu huyu? Tunaomba utuelekeze katika hili.

Jibu: Kinachotakiwa ni rekodini maneno yake darasani pasi na yeye kujua myaweke kwenye kanda kisha myapeleke Daar-ul-Iftaah. Mtu kama huyu hatakiwi kuachwa akawachezea watu. Hili ni wajibu kwako. Kwa kuwa kufanya hivi ni katika kuondosha maovu. Mtu kama huyu hatakiwi kuachwa akawachezea wanafunzi na akaeneza kati yao ukhurafi. Baya zaidi katika hayo ni kuwatukana kwake Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Huyu hatakiwi kuachwa kwa hali yoyote ile. Haifai kwenu kunyamaza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2120
  • Imechapishwa: 09/07/2020