Mwaliko wa anayefanya kazi benki

Swali: Binamu yangu anafanya kazi katika benki ya ribaa. Ameapa kwa Allaah ya kwamba hatokula wala kunywa nisipoenda katika mwaliko wake. Je, niitikie mwaliko wake na kutekeleza kiapo chake?

Jibu: Ikiwa unajua kuwa chakula chake hichi kinatokamana na pesa ya ribaa hii, usile katika chakula hicho hata kama ameapa kwa Allaah. Ikiwa hujui msingi ni kwamba ni halali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (71) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah26-07-1438h%20-%20Copy.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2017