Mwakilishwi amechelewesha Zakaat-ul-Fitwr


Swali: Kuna mtu alimpa Zakaat-ul-Fitwr mtu mwingine amtolee. Lakini aliyepewa kazi hii hakuitoa isipokuwa baada ya swalah ya ´Iyd. Je, inatakasika dhimma ya yule mtu wa kwanza?

Jibu: Ndio. Kama aliitoa dhimma yake inatakasika. Yule aliyepewa kazi hiyo kama alisahau na akachelewesha kwa sababu ya kusahau, hapana neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (87) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-3-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 20/11/2018