Swali: Je, mwajiriwa ana haki ya kuchukua pesa kutoka kwenye shirika lao kwa madai kwamba wamemdhulumu haki yake?

Jibu: Aombe haki yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Tekeleza amana kwa wale waliokuamini na usimhini mwenye kukuhini.”

Omba haki yako. Wasipofanya hivo, nenda mahakamani. Peleka mashtaka yako mahakamani. Usipoweza kufanya hilo la kwanza na hili la pili na unaweza kuchukua haki yako bila kumdhulumu yoyote, chukua haki yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (83) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-15-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/01/2018