Swali: Baadhi ya wanafunzi wanamjuzishia mwanamke hii leo kusafiri peke yake bila Mahram. Hoja yao ni kwamba safari haina siku moja wala mbili za kulala, kama ilivyokuja katika Hadiyth, na kwamba anaandamana na kundi la watu waaminifu. Ni vipi litajibiwa hili?

Jibu: Aseme anavyotaka, lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”[1]

Sema unavotaka, lakini sisi tunasema ya kwamba Mtume amesema hivi. Tuchukue maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au tuchukue maneno yako? Ni wajibu kwa mtu kumcha Allaah na asitoe mfano wa fatwa kama hizi.

Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni yenye kuenea na yanahusu zama zote; zama za punda, zama za ndege, zama za roketi. Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni yenye kuenea na ni yenye kutumika katika kila zama na mahali. Hatuyafuti kwa sababu ya kubadilika kwa mazingira. Haijuzu kwa mwanamke kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.

[1] al-Bukhaariy (1088) na Muslim (1339).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 17/09/2017