Muuzaji anabaki na malipo ya awali

Swali: Je, muuzaji ana haki ya kupewa malipo ya awali ikiwa biashara bado haijatimia?

Jibu: Kwa mujibu wa Ahmad na baadhi ya wengine inafaa kwa muuzaji kuchukua. Mnunuzi akiagiza bidhaa na kisha baadaye asiikomboe na hivyo akamzuia muuzaji kuiuza kwa wateja wengine, basi muuzaji atabaki na yale malipo ya awali kutokana na yale madhara yaliyosababishwa katika ule muda wa kusubiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (28)
  • Imechapishwa: 29/01/2022