Muumini anaweza kuadhibiwa kwa dhambi kubwa


Swali: Mtumwa wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye alichukua ngawira yuko Motoni na atadumishwa humo milele?

Jibu: Ni nani ambaye amekwambia kuwa atadumishwa humo milele? Hili ni kwa ajili ya matishio tu. Muumini anaweza kuingia Motoni kwa ajili ya dhambi kubwa. Muumini anaweza kuingia Motoni kwa ajili ya dhambi kubwa ikiwa Allaah hatomsamehe. Anaingia Motoni na anaadhibiwa ndani yake. Huenda akaadhibiwa mpaka akawa makaa kwa kuungua, kisha baada ya hapo akatolewa ndani ya Moto ilihali ni muumini. Anaadhibiwa kwa dhambi yake kubwa isipokuwa ikiwa kama Allaah Atamsamehe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (51) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-05-27.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014