Swali: Kuna mtu ametamka shahaadah hali ya kuwa ni mwenye imani safi, mkweli kutoka moyoni mwake na mwenye kujisalimisha. Lakini hakuwahi kabisa kufanya kheri maishani mwake pamoja na kwamba alikuwa na uwezo wa kufanya hivo. Je, anaingia chini ya utashi wa Allaah au ni kafiri?

Jibu: Ikiwa haswali basi ni kafiri japokuwa atatamka shahaadah. Lau angelikuwa ni mkweli kwa kutamka kwake shahaadah basi asingeliacha swalah. Kwa sababu swalah ndio mafungamano kati ya mtu na Allaah (´Azza wa Jall). Kumekuja dalili kutoka katika Qur-aan, Sunnah, mtazamo sahihi na maafikiano ya swalah (kama walivosimulia wengi) ya kwamba yule mwenye kuacha swalah ni kafiri na atadumishwa Motoni milele. Ni jambo haliingii chini ya utashi wa Allaah. Sisi hatuyasemi hayo kutoka vichwani mwetu, tunayasema hayo kutoka katika Qur-aan, Sunnah na maneno ya Maswahabah. ´Abdullaah bin Shaqiyq amesema:

“Hakuna kitu ambacho Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  walikuwa wanaonelea katika matendo kukiacha ni ukafiri isipokuwa swalah.”[1]

Haafidhw Ibn Raahuuyah amenukuu maafikiano ya Maswahabah juu ya kwamba yule asiyeswali ni kafiri.

Kuhusiana na matendo mengine mtu akiyaacha, yuko ndani ya utashi wa Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotaja adhabu ya mtu asiyetoa zakaah akasema:

“Kisha baada ya hapo ataona njia yake; ima kuelekea Peponi au Motoni.”[2]

Angelikuwa ni kafiri basi asingelipata bahati yoyote ya kuona njia yake ya kuelekea Peponi. Kadhalika inahusiana na swawm na hajj. Mwenye kuyaacha hakufuru; anaingia chini ya matakwa ya Allaah. Lakini hata hivyo ni katika watenda maovu makubwa.

[1] at-Tirmidhiy (2622). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

[2] Muslim (987).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-As-ilah al-Qatwariyyah, uk. 9-13
  • Imechapishwa: 03/02/2019