4- Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Masafa ya baina ya mbingu ya dunia na inayofuatia ni miaka 500. Baina ya kila mbingu mpaka nyingine ni miaka 500. Baina ya mbingu ya saba na Kursiy ni miaka 500. Baina ya Kursiy na maji ni miaka 500. ´Arshi iko juu ya maji na Allaah Yuko juu ya ´Arshi na hakuna kinachofichikana Kwake katika matendo yenu.

Ameipokea Ibn Mahdiy kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa ´Aaswim, kutoka kwa Zirr, kutoka kwa ´Abdullaah. al-Mas´uudiy amepokea mfano wahiyo, kutoka kwa ´Aaswim, kutoka kwa Abu Waa-iyl, kutoka kwa ´Abdullaah. Haafidhw adh-Dhahabiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Imepokelewa kwa njia nyingi.”

Yeye (Subhaanahu wa Ta´a) yuko juu ya viumbe Wake. Aliye juu, juu kabisa:

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ

”Naye ni Mwenye kudhibiti juu ya waja Wake.”[1]

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ

“Wanamuogopa Mola wao Aliye juu yao na wanafanya yale wanayoamrishwa.”[2]

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ

”Malaika na Roho wanapanda Kwake katika siku kipimo chake ni sawa na miaka khamsini elfu.”[3]

يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ

 “Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi nitakusinzisha na Mwenye kukupandisha Kwangu.”[4]

Kuna dalili nyingi ndani ya Qur-aan, Sunnah, akili na maumbile zinazoonyesha kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) yuko juu ya viumbe. Wapo ambao wamesema kwamba zimefika dalili elfumoja. Haafidhw adh-Dhahabiy ameandika juu ya maudhui haya na akakipa jina la ”al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar”. Kimechachapishwa na kinapatikana. Ndani yake ametaja dalili kuhusu uwepo wa Allaah juu ya viumbe Wake. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wameafikiana juu ya Allaah kuwepo juu ya viumbe kwa dhati Yake. Kwa ajili hiyo amesema:

“… na Allaah Yuko juu ya ´Arshi…. “

Bi maana ikiwa Allaah yuko juu ya viumbe na Allaah yuko juu ya ´Arshi, ni dalili inyoonyesha kwamba Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni wa juu na yuko juu kabisa ya viumbe Wake. Aidha viumbe wote ukivilinganisha na kiganja cha mkono cha Mwingi wa rehema ni kama chembe ya hardali katika kiganja cha mmoja wenu, kama ilivyotajwa katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Amesema:

“… na hakuna kinachofichikana Kwake katika matendo yenu.”

Msifikirie kuwa yuko mbali na waja Wake kwa sababu tu yuko juu ya viumbe Wake. Pamoja na ujuu Wake huu hakuna chochote kinachofichikana Kwake katika matendo ya wanadamu. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko juu ya ´Arshi na ujuzi Wake umeenea kila mahali. Hakuna chochote kinachofichikana Kwake:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ

“Hakika Allaah Hakifichiki Kwake chochote katika ardhi wala katika mbingu.”[5]

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

“Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho na Aliye juu na Aliye karibu – Naye juu ya kila jambo ni mjuzi. Yeye ndiye aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ‘Arshi; anajua yale yanayoingia ardhini na yale yatokayo humo na yale yanayoteremka kutoka mbinguni na yale yanayopanda humo – Naye yupamoja nanyi popote mlipo. Allaah ni Mwenye kuyaona yote myatendayo.”[6]

Bi maana kwa ujuzi Wake (Subhaanahu wa Ta´ala) na uzungukaji Wake. Hakifichikani chochote katika matendo yetu. Ni mamoja mema na ya shari. Anakijua kila kinachofanywa na waja Wake na hakuna kinachofichikana Kwake:

وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ ۚ وَمَا يَعْزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَلَا أَصْغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرَ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ

“Hushughuliki jambo lolote na wala husomi humo katika Qur-aan na wala hamtendi matendo yoyote isipokuwa Tunakuwa mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichiki kwa Mola wako hata cha uzito wa chembe katika ardhi wala mbinguni na wala kidogo kuliko hicho na wala kikubwa zaidi ya hicho isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha.”[7]

Asifikirie yeyote kwamba Allaah akiwa juu basi anakuwa mbali na viumbe Wake na kwamba hajui kuhusu matendo yao na hivyo akafikiria kuwa Muumbaji ni kama viumbe. Kiumbe akiwa sehemu iliyo juu basi hajui yaliyoko chini yake na kinachoendelea huko chini. Hii ni hali ya viumbe. Ama Allaah (Jalla wa ´Alaa) hakuna chochote kinachofichikana Kwake. Vovyote viumbe watavyokuwa wakubwa na wapana si chochote ukimlinganisha na Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala). Yeye ni Mwenye kuwazunguka, mwenye kuwajua na mwenye kuwaona. Anasikia yale wanayoendelea nayo, anayaona yale wanayoendelea nayo. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ni mjuzi wa kila jambo. Hakuna chochote kinachopitika isipokuwa kwa kupanga Kwake, kukadiria na kuamrisha Kwake. Yote haya yanafahamisha ujuu Wake, ujuzi na kuyazunguka Kwake mambo.

[1] 6:18

[2] 16:50

[3] 70:4

[4] 3:55

[5] 03:05

[6] 57:03-04

[7] 10:61

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 666-667
  • Imechapishwa: 09/09/2019