Muuaji muumini hatodumu Motoni milele

Swali: Vipi kuoanisha kati ya Aayah mbili ambapo ya kwanza inasema:

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا

“Na yeyote atakayemuua muumini makusudi, basi malipo yake ni Moto ni mwenye kudumishwa humo na Allaah atamghadhibikia na atamlaani na atamuandalia adhabu kuu.” (04:93)

na:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.” (04:48)

Swali: Muulizaji angesoma Aayah nyingine inayosema:

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

“Hakika yule atakayemshirikisha Allaah, basi hakika Allaah atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni motoni – na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kuwanusuru.” (05:72)

na ya pili isemayo:

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا

“Na yeyote atakayemuua muumini makusudi, basi malipo yake ni Moto ni mwenye kudumishwa humo na Allaah atamghadhibikia na atamlaani na atamuandalia adhabu kuu.”

Hakuna tofauti. Kudumishwa kwa washirikina ni kwa njia ya milele. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

“Hakika yule atakayemshirikisha Allaah, basi hakika Allaah atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni motoni – na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kuwanusuru.”

Kudumishwa huku ni kwa njia ya milele. Kuhusu mtu ambaye ameua:

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا

“Na yeyote atakayemuua muumini makusudi, basi malipo yake ni Moto ni mwenye kudumishwa humo na Allaah atamghadhibikia na atamlaani na atamuandalia adhabu kuu.”

maana yake ni kuwekwa Motoni muda mrefu kwa muda maalum. Kwa sababu kuua ni katika madhambi makubwa. Lakini mshirikina ni kudumishwa Motoni milele. Lakini muumini Motoni muda mrefu kwa muda maalum.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/ما-هو-الرابط-بين-الآيتينـمَنْ-يَقْتُلْ-مُؤْمِناً-مُتَعَمِّداً-والآيةإِنَّ-اللَّهَ-لا
  • Imechapishwa: 19/06/2022