Swali: Ni yapi maoni yako kwa mtu kama, Shaykh Safar al-Hawaaliy, ambaye anamtuhumu Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kwa Irjaa´?

Jibu: Amemdhulumu Shaykh al-Albaaniy. Naonelea kuwa Murji-ah wa sasa ni wafuasi wa Sayyid Qutwub. Wale wanaomtakasa Sayyid Qutwub na kutetea vitabu vyake ambavyo ndani yake kuna kuwasema vibaya baadhi ya Mitume na Maswahabah, Takfiyr juu ya Ummah na kwa baadhi ya Maswahabah, Wahdat-ul-Wujuud na Huluul na akawa na mapenzi juu ya mtu huyu na vitabu vyake. Nionavyo huyu ndiye Murji-ah aliyepetuka mipaka.

Shaykh al-Albaaniy ni Salafiy! Anafuata mfumo wa Salaf. Lakini wakati anapojadili, wakati mwingine huongea kwa njia ambayo sisi hatukubaliani nae. Hata hivyo, lau utasoma vitabu vyake vyote kuanzia mwanzo mpaka mwisho utaona tu jinsi gani anavyoweka wazi manhaj ya Salaf na kuwapiga vita Murji-ah. Soma aliyoandika ya mwisho kwenye footnote katika “adh-Dhabb al-Ahmad ‘alaa Musnad-il-Imaam Ahmad.” Soma ukurasa 32 na 33. Humo kumebainika ya kwamba mtu huyu anafuata madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kunapokuja katika imani na kwamba inapanda na kushuka na kwamba [´amali] ni katika imani. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Hata hivyo, baadhi ya mifano humo anaiongelea kimakosa, natumai kwa Allaah atamswamehe kwayo. Hatukubaliani nayo. Ilitokea mimi mwenyewe kumraddi kwayo wakati huohuo namheshimu, kumuadhimisha na kumpa udhuru. Nanimuomba Allaah Amswamehe na Kumrehemu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lubaab, uk. 503-504
  • Imechapishwa: 05/09/2020