Swali: Maneno ya Allaah (Subhaanah):

أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ

“Je, umemuona yule aliyefanya matamanio yake kuwa ndiye mwabudiwa wake?”[1]

Ni vipi matamanio yanakuwa mungu wa mtu? Hiyo ina maana kwamba anakuwa ni mwenye kuyaabudu na hivo anakufuru?

Jibu: Ina maana kwamba anafuata matamanio yake na kutii yale yanayomwamrisha matamanio na kumkataza. Hivi ndivo anayafanya matamanio kuwa mungu hali ya kumuamrisha na kumkataza. Hii ndio maana ya:

أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ

“Je, umemuona yule aliyefanya matamanio yake kuwa ndiye mwabudiwa wake?”

Lakini haina maana kwamba anakufuru. Maana yake ni kwamba anakuwa na upungufu katika imani na kufuata kwake. Hakuna yeyote katika sisi ambaye amesalimika na kufuata matamanio. Tumeshindana tu wamoja ni sana wengine kidogo.

[1] 45:23

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (81) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-1-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 01/04/2018