Mumewe amekufa na hajui ni watoto wepi aliyowafanyia ´Aqiyqah na wepi hakuwafanyia

Swali: Mimi ni mwanamke ambaye nimejaaliwa watoto sita wakiwemo wavulana na wasichana ambapo wane katika wao wakafa mwanzoni mwa umri wao na akabaki na mvulana mmoja na msichana mmoja. Baada ya hapo mume wake pia akafa ambaye hakuacha anawafanyia ´Aqiyqah isipokuwa wawili tu katika wao kwa sababu hakuwa na uwezo. Sijui ni wepi katika wao ambao hakuwafanyia ´Aqiyqah na ni wepi waliofanyiwa ´Aqiyqah. Nifanye nini sasa? Sijui hawa waliobakia ndio ambao walifanyiwa ´Aqiyqah au hapana?

Jibu: Hakuna linalomlazimu. Ambaye ni wajibu kufanya ´Aqiyqah ni baba. Kunapofika wakati wa ´Aqiyqah na yeye hana uwezo hukumu hiyo inaanguka kwake. Allaah haikalifishi nafsi isipokuwa vile inavyoweza. Ikiwa mwanaume ambaye hana mali hajj na zakaah kwake vinaanguka basi hili la ´Aqiyqah ni aula zaidi. Tunamwambia ikiwa pindi walipozaliwa baba yao hakuwa na uwezo wa kuwafanyia ´Aqiyqah hakuna kinachomlazimu. Na kama alikuwa ni tajiri ameacha kitu kimechopendekezwa.

Kuhusiana na mwanamke wewe na watoto wako hakuna kinachowalazimu kabisa. Si nyinyi wenye kuzungumzishwa inapokuja katika ´Aqiyqah. Mwenye kuzungumzishwa ni baba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (23)
  • Imechapishwa: 07/01/2019