Mume wangu anazungumza na wasichana na haniheshimu hata kidogo

Swali: Matatizo yangu na mume wangu ni kuhusu intaneti, kuzungumza na wasichana na kuhifadhi picha zao kwenye kompyuta. Hali kadhalika anatafuta picha za wanawake walio uchi. Vipi nitatangamana nae pamoja na kuwa yeye anajua anayoyafanya sio mazuri. Isitoshe haheshimu hata mimi nikiwa nae. Ananidharua kwa kiasi kwamba anazungumza na wasichana pindi mimi nakuwa karibu naye. Je hii ni sababu yenye kutosheleza kwa kutaka talaka kutoka kwake? Pamoja na kujua ya kwamba tuna mtoto ambaye kafikisha miezi minane. Naomba uninasihi?

Jibu: Ikiwa mume wako ni katika watu wema, mtu wa swalah, swawm, mtu wa ´ibaadah na wala hujui kutoka kwake yanayopingana na tabia njema, kama kuchanganyika na wanawake ambao ni ajinabi kwake au mambo ya haramu yaliyo ya wazi kabisa, kuwa na subira. Endelea kumnasihi na mfikishie salamu kutoka kwangu na kumwambia ya kwamba kitendo hichi ni khatari kwake. Huu ni mlango wa shaytwaan. Kunakhofiwa juu yake hali yake ikazidi kupeya mpaka akatumbukia katika kufanya machafu.

Ama ikiwa ni katika mafusaki, walio na mapungufu (makubwa), basi wakifikishie jambo wazazi wako ili watatua tatizo hili. Mambo yakifia mpaka kupata madhara, una haki ya kuomba kutenguka kwa ndoa au ukajivua katika ndoa.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/2863
  • Imechapishwa: 20/09/2020