Mume wake kamtupa miaka miwili na kwenda kutafuta elimu


Swali: Afanye nini mwanamke ambaye mume wake kamtupilia zaidi ya miaka miwili kwa hoja ya kwamba anatafuta elimu. Na mwanamke huyu kuna khatari akatumbukia katika fitina kwa kumkosa mume wake. Ipi hukumu ya hili?

Jibu: Mwanamke huyu akiweza kusubiri na ameachiwa matumizi na akapenda mwenyewe kusibiri, basi afanye hivyo. Ama akikhofia nafsi yake fitina, anaweza kuomba waachane.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=687
  • Imechapishwa: 24/02/2018