Mume wake anamlazimisha kinyume na maumbile wakati wa hedhi

Swali: Mume wangu ananilazimisha kufanya naye jimaa wakati wa hedhi. Wakati ninapombainishia uharamu wa hilo katika Qur-aan basi anakuwa mkali sana na anasema kwamba kukataa kwangu huku namsaidia juu ya kufanya haramu. Ni zipi nasaha zako kwa mwanamme huyu na mfano wake na wale wanamme wengine ambao huenda wakawalazimisha wake zao kuwaingilia kinyume na maumbile?

Jibu: Nasema:

وَمَن لَّمْ يَجْعَلِ اللَّـهُ لَهُ نُورًا فَمَا لَهُ مِن نُّورٍ

“Ambaye Allaah hakumjalia nuru, basi hawi na nuru.”[1]

Kumwingilia mwanamke wakati wa hedhi ni haramu. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ

“Waepukeni wanawake katika hedhi.”[2]

Ikiwa mume anataka kustarehe basi astarehe pasi na kumwingilia. Kwa mfano anaweza kustarehe naye kati ya mapaja yake au akayamaliza matamanivu yake kwa njia yoyote. Lakini hata hivyo asimwingilie kwenye uke wake.

Ama kumwingilia kwenye tupu ya nyuma ndio chafu zaidi. Ikiwa Allaah (Ta´ala) amekataza kumwingilia mwanamke ndani ya hedhi sehemu ile ya uke, ni vipi basi anaweza kujielekeza mpaka akamjamii sehemu hii chafu? Lakini huku ni kupinduka kwa maumbile. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Mwenye kutambulika kwa kitendo cha kumwingilia mwanamke kwenye tupu yake ya nyuma, basi ni wajibu kuwatenganisha kati yao.”

Anatakiwa kuponywa. Kwa sababu huyu anakiuka maharamisho ya Allaah na hakushukuru neema ya Allaah juu yake. Jambo ni lenye wasaa. Mtu anaweza kustarehe kati ya mapaja yake na akayamaliza matamanivu yake kwa kufanya hivo.

Kuhusu mwanamke ni lazima kwake kukataa pale atapomuomba kumwingilia wakati yuko na hedhi au kwenye tupu ya nyuma.

[1] 24:40

[2] 02:222

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (55) http://binothaimeen.net/content/1261
  • Imechapishwa: 07/06/2020