Swali: Mwanamke wa Ahl-us-Sunnah ameolewa na mume asiyependa Sunnah, anawachukia Ahl-us-Sunnah na kusema siku zote wale waliomuua ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) walikuwa na haki[1]. Unamnasihi nini?

Jibu: Ni katika Khawaarij na pengine Shiy´ah. Ima ni Khaarijiy au Shiy´iy. Ni lazima kwake kuomba kutengana ikiwa hatubu kwa Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Sayyid Qutwub amesema:

“Hatimaye kukajitokeza mapinduzi kwa ´Uthmaan. Haki na batili vikachanganyika, mazuri na mabaya vikachanganya. Lakini yule mwenye kuyaangalia mambo kwa mtazamo wa Kiislamu na kuyajua mambo kwa roho ya Kiislamu ni lazima aone kuwa mapinduzi yalikuwa ni kutokamana na roho ya Kiislamu.” (al-´Adaalah al-Ijtimaa´iyyah, uk. 160)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20%20-%204%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017