Swali: Mke katofautiana na mume wake katika jambo la Shari´ah. Yeye mke anaamini kuwa ni Haramu na mume anaamini kuwa inaruhusiwa. Mume anamuamrisha kukifanya. Je, mke amtii?

Jibu: Ikiwa kafikia daraja ya Ijtihaad, atakuwa ni mwenye kufanya ´Ibaadah kwa ufahamu wake na Ijtihaad yake. Ama ikiwa ni mwanamke anayefuata matamanio yake, ni juu ya mume kumpiga. Kwa mfano kamwambia: “Usitoke, usijishauwe naye anajishaua na anasema kuwa kujishaua kunajuzu”. Hivyo, ikiwa ni ambaye kafikia Ijtihaad, hapana asimpige kwa kuwa atakuwa ni mwenye kufanya ´Ibaadah kwa Ijtihaad yake na si juu yake mume kumlazimisha. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Nawausia kuwatendea wema wanawake.”

Miongoni mwa kuwatendea wema, ni yeye mume kumshaji´isha juu ya kufahamu Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama Kauli Yake (Ta´ala):

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya (matumizi) wanayotoa katika mali zao. Basi wanawake wema watiifu, wenye kuhifadhi (hata) wanapokuwa hawapo (waume zao) kwa Aliyoyahifadhi Allaah.” (04:34)

Aayah hii, makusudio yake ni katika jambo lisilokuwa hili ambalo ni masuala ya Ijtihaad. Pengine akawa ni mtafutaji elimu, anajua kiarabu, Hadiyth za Mtume wa Allaah, Kitabu cha Allaah na kwa mfano anaona kuwa kuweka mkono wa kulia juu ya kifua baada ya Rukuu ni Sunnah, na yeye mume anaona kuwa sio Sunnah, ni juu ya kila mmoja kufanya vile anavyoona na yasiyokuwa hayo, hili linatumika hata ikiwa ni katika masuala ambayo mume anaona kuwa ni Haramu na mke anaona kuwa inaruhusiwa kutokana na Ijtihaad yake. Ikiwa mke ni mjinga, ni juu yake kumfunza na yeye mume ataulizwa kwa alichokichunga.

“Kila mmoja wenu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga.”

Swali: Ikiwa ni katika masuala ya kufunua uso. Mke anaona kufunua uso ni jambo linajuzu. Je, mume amkataze?

Jibu: Asimkataze [ikiwa mwanamke kafikia daraja ya Ijtihaad]. Akiweza kumsubiria ni jambo zuri, la sivyo aachana nae. Ikiwa hawezi kuvum-ilia, si juu yake kumkataza. Ingawa na sisi tunaona kuwa ni wajibu kwake kufunika uso wake, kutokana na Hadiyth zilizotangulia:

“Mwanamke ni ´Awrah (uchi).”

Na Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ

“Ee Nabii! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jalaabiyb zao.” (33:59)

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://firqatunnajia.com/mume-na-mke-wanatofautiana-katika-masuala-ya-dini
  • Imechapishwa: 26/02/2018