Mume kuoa mwanamke mwingine ndani ya eda ya mke wake


Swali: Mtu kama alikuwa na mke akamtaliki. Je, anaweza kumuoa dada yake ndani ya eda yake (huyo mke wake)? Na akifa anaweza kuoa katika hali hii?

Jibu: Akimtaliki mke wake, haijuzu kwake kumuoa dada yake wala wanawake wengine isipokuwa baada ya eda, baada ya kwisha kwa eda. Ikiwa ni Talaka rejea, hili wamekubaliana wanachuoni wote. Ya kwamba haijuzu kwake kumuoa dada yake wala mwanamke mwingine yeyote isipokuwa baada ya kwisha kwa eda, kwa kuwa mwanamke rejea ni mke. Ama ikiwa ni Talaka Baain [Talaka ambayo kakosa haki ya kumrejeakwa kuwa eda imekwisha], au Talaka kwa mwanamke kujivua (katika ndoa), hapa kuna tofauti, lakini kauli yenye nguvu ni kuwa asioe mwingine ila baada ya kwisha kwa eda. Ama (mke) akishakufa, hakuna ubaya akaoa mwanamke mwingine baada ya siku moja au mbili tokea siku ile kafariki. Ikiwa mke kafa, eda yake imekwisha kwa kufa kwake, ndoa imekwisha kwa kufa kwake. Katika hali hii, hakuna ubaya akamuoa dada yake au mwanamke mwingine yeyote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb