Mume kumuosha mke wake anapokufa na msichana mdogo


Swali: Ni sahihi kwa mwanaume kumuosha mke wake anapokufa au msichana wa mwaka moja mpaka miwili hata kama atakuwa ni ajinabi kwake?

Jibu: Hakuna ubaya wowote mwanaume kumuosha mke wake, na mke kumuosha mume wake kwa kufuata Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama kinyume na mke, hapana. Lakini mdogo ni kama mfano wa mke. Hakuna ubaya mwanaume akamuosha msichana mdogo, na wala hakuna neno akamuosha kama mke. Ama mama yake, msichana wake, dada yake na mfano wa hao, haifai kwake kuwaosha. Bali hawa wanaoshwa na wanawake. Lakini msichana ambaye ni mdogo haina neno anaweza kuoshwa na wanaume. Ikiwa ni chini ya miaka saba; kama mfano wa msichana wa miaka mitano, tatu, mine, haina neno.

Hali kadhalika, mvulana wa chini ya miaka saba anaweza kuoshwa na wanawake pia. Watoto chini ya miaka saba wanaweza kuoshwa na wanaume na wanawake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 22/03/2018