Mume kumtaliki mke wake katika twahara aliyomjamii

Swali: Je, inafaa kwa mwanaume kumtaliki mke wake katika twahara ambayo amemjamii?

Jibu: Hapana, haijuzu ikiwa sio katika wale wanawake waliokoma hedhi na wanajiwa na ada ya mwezi. Lakini akiwa amekwishakoma hedhi au mjamzito basi hapana vibaya kumtaliki katika twahara yake. Ama akiwa anapata ada na anachelea kushika ujauzito basi asimtaliki mpaka ajue kwanza kama ana mimba au anapata hedhi kisha akasafika. Baada ya hapo ndio amtaliki kabla ya kumwingilia. Hivi ndivo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomwamrisha Ibn ´Umar.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21604/هل-يجوز-للرجل-الطلاق-في-طهر-جامع-فيه
  • Imechapishwa: 28/08/2022