Mume kucheza na mke kwa kuiga sauti yake na anavyotembea


Swali: Baina yangu mimi na mke wangu kunapitika mzaha jambo ambalo linapelekea kumuiga anavyotembea na sauti yake. Nafanya hivyo kwa ajili ya maskhara na mzaha. Je, hili linaingia katika Kauli ya (Jalla wa ´Alaa):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ

“Enyi mlioamini! Watu (wanaume) wasiwadharau watu (wengineo, kwani) huenda (waliodharauliwa) wakawa bora kuliko wao.” (49:11)

JIbu: Usifanye hivyo. Allaah Akubariki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kamlaani mwanaume anayejifananisha na wanawake. Na kamlaani mwanamke anayejifananisha na wanaume.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/vhiWeeg0zLY
  • Imechapishwa: 18/03/2018