Swali: Je, ni lazima kwa mume kwenda na mke wake kuhiji ili awe Mahram wake ikiwa mume tayari amekwishahiji hapo kabla?

Jibu: Sio lazima. Isipokuwa ikiwa mke alimuwekea sharti hiyo. Vinginevyo hajj itakuwa ni lazima kwake punde tu atapopata Mahram. Ikishindikana mwanamke atoe katika mali yake ikiwepesika kufanya hivo mtu mwengine amuhijie. Ni katika kumtendea wema. Isipokuwa ikiwa alimuwekea sharti wakati wa kufunga ndoa kwamba atahiji pamoja naye.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14)
  • Imechapishwa: 31/05/2020