Mume kamtaliki mke wake mara sita kisha anasema kuwa hakumbuki

Swali: Kuna mwanamke kumuacha mume wake na kwenda katika nyumba ya dada yake hali ya kuwa yuko na watoto na baba yake. Mume wa dada yake akataka kuwasuluhisha. Alipotaka kufanya hivyo, akasema mke kuwa hatorudi kwake kwa kuwa ameshamtaliki mara sita na mimi kwake ni kama ajinabi. Na pindi ninapomkumbusha (mume juu ya Talaka hizo) anasema kuwa hakumbuki. Je, kufuatwe kauli ya mke au mume?

Jibu: Ni juu ya mwenye kudai abainishe na mwenye kukanusha ale yamini. La dhahiri ni kuwa mume ndio mwenye kudai, kwa kuwa yeye ndio kamtaliki. Kutokana na hili, ni juu yake kuleta mashahidi ya kuwa kamtaliki. Na kama hakufanya hivyo, hana jengine ila kula yamini. Hili ndio la dhahiri. Ama yaliyo baina yake (mke) na Allaah, akijua kweli kuwa kamtaliki zaidi ya mara tatu, haijuzu kwake kumpa kitu. Kwa kuwa akifanya hivyo atazingatiwa anazini nae.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1644