Swali: Mume wangu haswali na anasafiri sana kwenda katika miji ya maharibifu na pumbao…

Jibu: Kwa hali yoyote mume asiyeswali si sahihi kwa mke kubaki naye. Kwa sababu kuacha swalah ni ukafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yeyote atakayeiacha amekufuru.”

“Kati ya mtu na kufuru au shirki ni kuacha swalah.”

´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hana fungu katika Uislamu kwa yule mwenye kuacha swalah.”

Mume huyu hana kheri. Kwa masikitiko makubwa waume wengi wanakuwa namna hii. Utu wao kabla ya ndoa wanakuwa ni wafanyaji wakubwa wa ´ibaadah. Lakini baada ya kuoa tu utu wao unabadilika na wanakuwa na utu mwingine.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Maraatib-ul-Ihsaan 02 https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-09/mratib2.mp3
  • Imechapishwa: 27/09/2022