Swali: Mwamamke akitaka kujisitiri kwa Hijaab na mume wake au mmoja katika ndugu zake anamkataza, pamoja na kuwa anayefanya hivyo ni katika wanaoswali. Je, unamnasihi nini?

Jibu: Tunamchomnasihi mume huyu, anatakiwa kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ambaye Kamjaalia mke mwema ambaye anapenda Hijaab. Badala yake, anatakiwa amshaji´ishe juu ya hili. Kuwaangalia wanawake ni fitina. Ni fitina juu yao wanawake na vile vile ni fitina kwa yule mtazamaji. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Wanawake ni wapungufu wa akili na Dini… “

Na anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Sijaacha fitina iliokuwa kubwa baada yangu kwa wanaume kuliko (fitina ya) wanawake.”

Na ni Haramu kwake mume kumkataza. Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Mwanamke ni ´Awrah (uchi), Pindi anapotoka nje, matumaini ya Shaytwaan huongezeka.” (Kaipokea at-Tirmidhiy, Hadiyth ya ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´ahu)

Haijuzu kwake kumkataza, kama tulivyotangulia kusema. Hali kadhalika, mwanamke huyu haitakiwi kwake kumtii juu ya hili. Ajisitiri kwa Hijaab. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: “Utiifu ni katika mema.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1401
  • Imechapishwa: 26/02/2018