Swali: Dada huyu anasema. Mume wake anapuuzia swalah na anamnasihi. Wakati mwingine anamuuliza: “Je, umeswali?”. Anasema: “Je, kwa nini? Kwani umeona mimi ni kafiri?” Anauliza, je, juu yangu nina dhambi? Je, niishi naye na tumeshakuwa na watoto? Kula na kunywa nyumbani kwake ni haramu?

Jibu: Ikiwa ameacha swalah moja kwa moja na haswali kabisa, si pamoja na mkusanyiko wala nyumbani – anaacha swalah kwa kukusudia – haijuzu kwako kubaki pamoja naye. Bali ni wajibu kwako kumuomba kutengana naye. Ama ikiwa haachi swalah, anaswali lakini haswali pamoja na mkusanyiko wakati fulani, huu ni uvivu. Ameacha jambo la wajibu na anapata madhambi kwa kufanya hivyo na anamuasi Allaah. Lakini hili halipelekei kufarikana naye na kuishi kwake, pamoja na kuendelea kumnasihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls–1429-01-21.mp3
  • Imechapishwa: 17/09/2020