Mume anapewa thawabu kwa kumvumilia mke wake?

Swali: Kuwa na uvumilivu juu ya mke, tabia yake, ujinga wake na ukasumba wake mume anapewa thawabu kwa hilo?

Jibu: Ndio. Hili Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliliamrisha. Awe na subira juu ya mke wake kutokana na baadhi ya tabia yake akilinganisha kutokana na kheri inayopatikana kwake. Kheri yake ni nyngi zaidi. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muumini mwanaume asimchukie muumini mwanamke. Akichukia kutoka kwake tabia fulani ataridhia nyingine.”

Hakuna mwanamke mkamilifu asiyekuwa na kasoro, hakuna. Lazima awe na kitu fulani.

“Mwanamke ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja – na kuuvunja kwake ni kule kumpa talaka… “

Namna hii ndivyo anavyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13668
  • Imechapishwa: 20/09/2020