Mume anapata dhambi asipompa idhini mkewe kwenda kuhiji?


Swali: Je, mume anapata dhambi akimkatalia mke wake kuhiji?

Jibu: Ndio, anapata dhambi. Akimkatalia kufanya hajj ambayo imekamilisha sharti zake ni mwenye kupata dhambi. Kwa mfano mke anamwambia niko na Mahram wa kusafiri naye, niko na matumizi yangu na sitaki kutoka kwako pesa hata moja na wakati huohuo bado hajahiji hajj ya faradhi, katika hali hii ni wajibu kwake kumpa idhini. Asipompa idhini, basi ahiji japokuwa ni pasi na idhini yake. Isipokuwa ikiwa kama mke atakhofia kuwa atampa talaka. Katika hali hiyo mwanamke huyu atakuwa ni mwenye udhuru.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1409
  • Imechapishwa: 13/12/2019