Mume anamtilia uwazi mmoja katika wakeze kwamba hawezi kufanya uadilifu


Swali: Ni ipi hukumu mume akisema kumwambia mke:

“Ni sawa ukitaka kubaki na watoto wako. Vinginevyo nenda kwa familia yako na huna lolote kuhusiana na mimi.”?

Jibu: Akimpa khiyari namna hii ameitakasa dhimma yake. Kwa ajili hii Sawdah bint Zam´ah (Radhiya Allaahu ´anhaa), ambaye ni mmoja katika mama wa waumini, wakati alipokhofia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asije kumtaliki alimzawadia zamu yake ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ili apate kubaki pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikawa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamgawia ´Aaishah siku yake na ile siku ya Sawdah. Mwanaume huyu akimpa khiyari na kumwambia kwamba hawezi kufanya uadilifu baina yao; ima unisamehe na nitakasike, nikutaliki, nikuruhusu kwenda kwa familia yako na mfano wa hayo. Yakipatikana mambo hayo imetakasika dhimma yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (13) http://binothaimeen.net/content/6779
  • Imechapishwa: 09/02/2021