Swali: Mke wangu ana akaunti yake mwenyewe ya benki. Wakati mali yake inatimiza mwaka mmoja mimi humtolea zakaah kutoka kwenye mali yangu mwenyewe. Je, kitendo hichi kinafaa au ni lazima ajitolee zakaah kutoka katika pesa yake mwenyewe?

Jibu: Kumtolea inafaa lakini hata hivyo ni lazima amjulishe ili anuie. Katika hali hii wewe unazingatiwa unamuwakilisha. Ni lazima anuie kutoa zakaah kwa ajili ya nia. Vinginevyo inafaa, hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (18) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtfq-15011435-01.mp3
  • Imechapishwa: 08/11/2019