Swali: Mume wangu aliweka nadhiri kwamba hatooa mke mwingine midhali bado niko pmaoja naye. Je, ni lazima kwake kutekeleza nadhiri hii au hapana?

Jibu: Nadhiri hii ina hukumu ya yamini. Ni katika mlango wa kuweka nadhiri kwa sababu ya haja na ghadhabu kwa mujibu wa vile Fuqahaa´ walivyoiita. Kwa sababu aliweka nadhiri kwa kusudio la kujizuia peke yake. Akitaka kuongeza mke mwingine na bado yuko na mke wake, basi inafaa kwake kufanya hivo. Lakini hata hivyo afanye kafara ya yamini; kwa kulisha mafukara kumi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (05) http://binothaimeen.net/content/6682
  • Imechapishwa: 29/10/2020