Swali: Mimi ni mwenye kufunga deni langu la Ramadhaan. Mume wangu alinita kitandani pamoja na kuwa nilimtaka idhini kabla ya kuanza kufunga. Lakini akaendelea kung´ang´ania. Je, ninalazimika kutoa kafara?

Jibu: Si lazima kutoa kafara. Isipokuwa kwa yule aliyefanya jimaa mchana wa Ramadhaan na wakati huohuo akawa miongoni mwa wale ambao wamewajibika kufunga. Kulipa hakuna kafara ndani yake. Lakini haijuzu kwake mwanamke kumuitikia mume wake ikiwa kabla ya kuanza kufunga alipata idhini yake. Kwa sababu pale alipoanza kufunga swawm imefika inakuwa ya wajibu. Ni ya wajibu kwa sababu mume ndiye kamruhusu. Hana hoja yoyote. Ni haramu kwa mume kumwita kitandani ilihali amefunga swawm ya wajibu baada ya idhini yake. Hana udhuru wowote.

Lakini iwapo angefunga pasi na idhini yake angekuwa na haki ya kumwita na mke hana haki ya kumkatalia. Kwa sababu haki ya mume katika hali hii bado ni yenye kubaki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1621
  • Imechapishwa: 05/05/2018