Swali: Mume wangu alinijamii katika mchana miongoni mwa michana ya Ramadhaan na mimi nikiwa na hedhi na mume wangu amefunga. Ni ipi hukumu?

Jibu: Swali hili lina mambo mawili:

1- Kuhusu mume kumjamii mchana wa Ramadhaan. Ni lazima kwa mume wake kulipa na kutoa kafara pamoja pia na kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Atatakiwa kulipa siku moja badala ya siku ambayo alifanya jimaa.

Ama kafara ni kuacha mtumwa huru, asipopata basi afunge miezi miwili mfululizo, asipoweza basi alishe masikini sitini.

Hakuna chochote kinachomlazimu mwanamke. Kwa sababu hana ulazima wa kufunga kutokana na hedhi.

2- Amemjamii mke wake akiwa na hedhi. Ni lazima kwake kutoa dinari au nusu yake kutokana na Hadiyth ya Ibn ´Abbaas:

”Aitoe swadaqah danari au nusu yake.”[1]

Ameipokea Ahmad, at-Tirmidhiy na Abu Daawuud ambaye amesema:

“Namna hii ndivo ulivo upokezi Swahiyh.”

Makusudio ya dinari ni uzani wa dhahabu au thamani yake katika fedha.

Mwanamke huyu ikiwa alikuwa mwenye kutii basi nay eye atatiwa kutoa kafara kama mwanamme. Wote wawili wanatakiwa kutubu kwa Allaah kwa kitendo cha kufanya jimaa.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Ghudayyaan

´Abdullaah bin Maniy´

[1] Ahmad (01/237), Abu Daawuud (01/181), at-Tirmidhiy (01/245) na wengineo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (305)
  • Imechapishwa: 25/04/2020