Mume akifa ni lazima kwa mwanamke kuolewa na nduguye mume?

Swali: Inajuzu kwangu kuolewa na mwanaume ambaye sio ndugu wa mume wangu ilihali tayari nina watoto watatu pamoja naye? Ikiwa inafaa Kishari´ah inajuzu kwangu kusafiri nje ya nchi kutokea Misri na kwenda kwa mfano Saudi Arabia au Yemen kwa sababu huko kuna ndugu waliokuja kwa ajili yangu. Lakini hata hivyo nitaandamana na watoto vilevile.

Jibu: Mosi: Mwanamke anapofiliwa na mume wake na akakamilisha eda yake basi inafaa kwake kuolewa na yule ambaye anaona ana manufaa na yeye upande wa dini, amana na tabia. Haijalishi kitu ni mamoja awe ndugu wa huyo mume wake aliyefariki au mwengine.

Pili: Ni haramu kwa mwanamke kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.  Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”[1]

Kumeafikiwa juu yake.

[1] al-Bukhaariy (1088), Muslim (1339), at-Tirmidhiy (1170), Abu Daawuud (1723) na wengineo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (18/19)
  • Imechapishwa: 04/08/2017