al-Halabiy amesema:

“Mambo yakibambana kwetu na tukatofautiana juu ya fulani, haijuzu kabisa kufanya tofauti za wengine ikawa ni sababu ya sisi kutofautiana. Tukifanya hivo basi wapinzani watafaidi sana katika hilo.”

Tunatakiwa kuwa na umoja katika kitu gani? Si katika haki? Ndio. Mtu akienda kinyume na haki basi ni lazima kwetu kumnasihi. Ima ajirudi au tunamzingatia kama mpindaji na kumtulipia mbali. Akiwepo mtu mwenye kumsapoti na kumsaidia juu ya batili zake, tunamkemea na kumkata huyo msapotaji. Hili ni khaswa pale ambapo ikiwa mtu huyo mpindaji ana Bhid´ah za wazi kabisa na zenye madhara kama Bid´ah za khawaarij. Haitupasi kwetu kumnyamazia Mumayyi´iy huyu eti kwa sababu tunataka kuwafanya watu wawe na umoja. Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote juu ya kwamba Bid´ah za Khawaarij ni zenye madhara katika dini. Tukisema kuwa inajuzu kusoma kwa mtu Khaarijiy basi tunasaidia kuiobomoa dini na kuwashaji´isha waenezaji ufisadi.

Tuliwahi kuwa na Takfiyr, milipuko na uharibifu kabla ya baadhi ya vijana kuanza kusoma kwa watu kama hawa na kuwasapoti? Haijuzu kwetu kusema kuwa watu hawa wamehifadhi Qur-aan na wana elimu. Ni bora kuwa mjinga kuliko kuchukua elimu kutoka kwa watu hawa.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Durar an-Najmiyyah fiy Radd-ish-Shubuhaat al-´Aqadiyyah wal-Manhajiyyah, uk. 381-382
  • Imechapishwa: 18/03/2017