Muda mwingi mbele ya TV na kupuuza familia yake

Swali: Mume wangu alitaka kuleta king´amuzi/dishi juu ya watoto wangu ambapo mimi nikamkatalia. Lakini hata hivyo akaileta na kuiweka kwenye chumba mahali pa kupumzikia kwa nje. Matokeo yake akawa anatazama kila wakati mpaka kulala na kula tukawa tunahudhuria katika chumba hichi. Akawakata watoto wake na kukaa nao mpaka masomo yakalalamika juu ya kudhoofika kwao. Tabia yake ikawa inazorota kwa kitu kidogo tu. Siku alinifukuza nyumbani ambapo nikalala kwa jirani kwa sababu familia yangu inaishi al-Madiynah an-Munawwarah. Hivi sasa niko kwa familia yangu. Nifanye nini khaswa ukizingatia kwamba nimeshazaa naye watoto kama nilivyotaja.

Jibu: Hapana shaka kwamba haki iko na mwanamke huyu. Midhali hali imefikia kiasi cha kwamba mwanaume huyu amepinduka juu ya dishi hii. Haki iko pamoja na mwanamke. Lililo la wajibu kwa mwanaume huyu – mambo yakiwa kama alivosema mwanamke huyu – basi amche Allaah juu ya nafsi yake. Aivunje dishi hii. Kwa sababu inamzuia kutokamana na kumtii Allaah, kutangamana na familia yake, kuwaangalia watoto wake na manufaa mengine makubwa. Hivyo basi amche Allaah. Namuomba Allaah pale tu ataposikia maneno yangu basi amche Allaah na akivunje kifaa hichi ambacho kimepelekea katika hali hii iliyotajwa na mwanamke. Akifanya hivo basi maisha yake yatakuwa mazuri, moyo wake utapata utulivu, mambo yatakuwa mazuri na Allaah kuwakusanya yeye na familia yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Firqatunnajia.com Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (75) http://binothaimeen.net/content/1746
  • Imechapishwa: 07/09/2020