1- Tazama jinsi Fawziy al-Bahrayniy anavyowanukuu Ahl-us-Sunnah:

“Imani ni maneno na vitendo, inazidi na kupungua.”

Matamshi ya maimamu hawa hayakumshtua yeye kufaradhisha na kuwajibisha nyongeza:

“Imani inashuka mpaka hakubaki katika imani chochote.”

Matamshi haya hayakumshtua kuwafayia Tabdiy´ wale wasioitaja. Maimamu hawa wakiwemo Maswahabah ni wazushi na Murji-ah kwa mujibu wa Haddaadiyyah na ´Aqiydah yao. Allaah awaue wajinga, wenye kudhulumu na matamanio!

2- Sisi tunasema yale yanayosemwa na maimamu na Ahl-us-Sunnah katika wale walioeshi katika zama za Imaam Harb na wale walioeshi kabla yake. Tunaamini yale yote waliyokuwa wakiamini katika kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake, Qiyaamah, Pepo, Moto, adhabu na neema za ndani ya kaburi. Tunaamini majina na sifa za Allaah na matendo Yake. Tunayathibitisha kama yalivyotajwa katika Qur-aan na Sunnah. Tunaamini yale yote yanayofahamishwa na maandiko haya pasi na kushabihisha, kufananisha, kupotosha wala kukanusha. Tunayaamini haya na mengineyo katika yale Maswahabah na Salaf waliyokuwa wakiamini.

3- Tunaamini kuwa imani ni maneno na vitendo; maneno ya moyo na vitendo pamoja na matendo ya moyo na viungo vya mwili. Hatuendi kinyume na chochote katika waliokuwa wakiamini. Tunasema kama walivyosema Imaam Harb:

“Mwenye kwenda kinyume na chochote katika I´tiqaad hizi, akayatukana au akamkosoa yule mwenye kuyaamini, ni mzushi ambaye ameacha mkusanyiko na amepinda na mfumo wa Sunnah na njia ya haki. Hii ndio I´tiqaad ya Ahmad, Ishaaq bin Ibraahiym bin Makhlad, ´Abdullaah bin az-Zubayr al-Humaydiy na Sa´iyd bin Mansuur.

4- Hapo tunaongeza Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy, Muslim bin al-Hajjaaj, Abu Haatim ar-Raaziy, Abu Zur´ah ar-Raaziy, ´Abdullaah bin Ahmad, al-Khallaal ambao walikusanya elimu ya Ahmad na ya wengine walioiga mwongozo wao mpaka hii leo.

5- Tunasema kama walivyosema:

“Imani ni maneno na vitendo, nia na kushikamana na Qur-aan na Sunnah. Inazidi na kupungua. Wanachuoni wameshikamana na imani.”

6- Tunasema kama walivyosema:

“Mwenye kudai kuwa imani ni maneno pasi na matendo ni Murj-iy. Mwenye kudai kuwa imani ni maneno na matendo yamewekwa katika Shari´ah ni Murj-iy.”

Kwa kusema hivo wanakusudia kwamba matendo sio katika imani kwa mujibu wao.

7- Tunasema kama walivyosema:

“Mwenye kudai kuwa imani haipandi na wala haishuki ni Murj-iy. Mwenye kusema kuwa imani inapanda na wala haishuki ameafikiana na Murji-ah.”

8- Tunaamini yale yote yaliyosemwa na Imam Harb katika ilani yake.

9- Atayeninasibishia mimi au ndugu zetu katika Ahl-us-Sunnah I´tiqaad hizi batili ambazo wenye nazo wametuhumiwa na maimamu ametusemea uongo na kutuzulia.

10- Ni ajabu kuona mpumbavu huyu anataja matamshi ya Imaam Harb na ya wengine ili kutaka kuwafanya watu waelewe kuwa sisi tunaenda kinyume na uelewa wa Salaf katika imani na hukumu zao juu ya Ahl-ul-Bid´ah wakiwemo Murji-ah. Hakukoma katika mpaka huu batili na wa dhuluma. Amevuka zaidi ya hapo na kututuhumu kuwa sisi ni Raafidhwah, Khawaarij, Baatwiniyyah na Murji-ah.

Salafiyyah iko wapi ukilinganisha na Haddaadiyyah? Uko wapi uadilifu, inswafu, heshima na mapenzi ya Ahl-us-Sunnah ukilinganisha na kundi hili kandamizi?

 

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 37-38
  • Imechapishwa: 09/10/2016