Muislamu kumrithi anayefanya kufuru kubwa na asiyeswali

Swali: Je, inafaa kwa muislamu kumrithi mtu ambaye anatufu pembezoni mwa makaburi na anayaomba msaada? Je, inafaa kwa muislamu kumrithi asiyeswali?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh iliopokea al-Bukhaariy na Muslim:

“Haifai kwa muislamu kumrithi kafiri wala kafiri kumrithi muislamu.”

Haifai kwa ambaye anayazunguka makaburi, anayaomba uokozi na msaada kurithi kutoka kwa muislamu kama ambavo haifai kwa muislamu kumrithi kutokana na Hadiyth hii Swahiyh. Hakika si venginevyo huyu ambaye anayazunguka makaburi inafaa kwake kuwarithi watu mfano wake ambao ni waabudia makaburi. Kwani wao ni makafiri mfano wake. Muislamu anawarithi waislamu wenzie. Muislamu anawarithi waislamu na si makafiri. Na vivyo hivyo kinyume chake kafiri anamrithi kafiri na si muislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Haifai kwa muislamu kumrithi kafiri wala kafiri kumrithi muislamu.”

Ni Hadiyth ya Usaamah (Radhiya Allaahu ´anh).

Vivyo hivyo ambaye haswali. Kwani maoni yenye nguvu ni kwamba ni kafiri ambaye amekufuru ukafiri mkubwa. Wapo baadhi ya wanazuoni wameona kuwa ni ukafiri mdogo na si mkubwa muda wa kuwa anakubali kuwa ni lazima na hapingi uwajibu wake. Lakini maoni sahihi ni kwamba ni ukafiri mkubwa na kwamba wale warithi wake waislamu hawatorithi kutoka kwake. Mirathi yake itapelekwa katika wizara ya mambo ya fedha ya waislamu (بيت المال). Kwa sababu ameritadi kwa kitendo hicho. Isipokuwa kama ana ndugu zake wenye hali kama yake ya kuacha swalah. Katika hali hiyo wao ndio watamrithi kama ambavo inafaa kwa makafiri kurithiana wao kwa wao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/253) https://binbaz.org.sa/fatwas/19305/19305/لا-يرث-المسلم-الكافر-ولا-الكافر-المسلم
  • Imechapishwa: 20/04/2021