Swali: Je, muislamu akila pamoja na mnaswara au makafiri wengineo au akanywa pamoja naye inazingatiwa kitendo hicho ni haramu? Ikiwa ni haramu tunasemaje kuhusu maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَهُمْ

“Chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu na chakula chao ni halali kwao.”[1]?

Jibu: Kula pamoja na kafiri sio haramu mtu akihitajia kufanya hivo au manufaa yanayokubalika Kishari´ah. Lakini usiwafanye marafiki ukala pamoja nao pasi na sababu inayokubalika Kishari´ah au manufaa yanayokubalika Kishari´ah. Usianasike na kufurahi pamoja nao. Lakini haja ikipelekea kufanya hivo, kama mfano wa kula pamoja na mgeni, kuwalingania katika dini ya Allaah na kuwaelekeza katika haki au kwa sababu zengine zinazokubalika Kishari´ah hakuna neno.

Sisi kuhalalishiwa chakula cha Ahl-ul-Kitaab haina maana kuwafanya marafiki na wenye kukaa nao. Wala haina maana ya kushirikiana nao katika kula na kunywa pasi haja wala manufaa yanayokubalika Kishari´ah.

[1] 05:05

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/old/38099
  • Imechapishwa: 12/11/2019