Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanaume wenye kujifananisha na wanawake na wanawake wenye kujifananisha na wanaume. Je, kunaingia mavazi ya kubana?

Jibu: Inahusiana na mavazi maalum kwa wanawake. Mwanaume akiyavaa anakuwa ni mwenye kujifananisha na anaguswa na laana. Hakuingii ndani yake mavazi ambayo sio maalum kwa wanawake. Lakini hata hivyo ikiwa ni yenye kubana hayajuzu na sio kwa sababu ni ya wanawake. Hata mwanamke na yeye haijuzu kwake kuvaa mavazi ya kubana. Wanawake wa Kiislamu hawavai mavazi ya kubana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-09.mp3
  • Imechapishwa: 08/06/2020