Swali: Sisi tupo katika mji wa Kiislamu na kumekuwa fitina kubwa baina ya watawala na raia wanaofanya maandamano. Tunapowaambia kuwasikiliza na kuwatii watawala hawatusikii. Mnatunasihi nini?

Jibu: Mtu anapaswa kufuata haki sawa watu wakiafikiana naye au hapana, atashikamana na haki na uongofu sawa watu wakikubali au wakikataa.

Kwa wale watu ambao wamekataa kabisa, tayari wako thabiti kuendelea kufanya hayo maandamano, na hawakubali ila kutaka kukabiliana kwa jambo ambalo litakuja kuleta madhara. Mtu anatakiwa awe na msimamo katika kumtii Allaah. Na ikiwa baadhi ya watu wamesimama na jambo ambalo Muislamu hatakiwi kuwa humo – mtu asiwe na watu hawa. Mtu ashikamane na haki hata kama si watu wengi watakusikiliza.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=BkLmz-8aB1Q
  • Imechapishwa: 06/09/2020