Swali: Ni vipi kuoanisha kati maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya Muhrim:

“Kwani hakika Allaah atamfufua siku ya Qiyaamah hali ya kuwa ni mwenye kuleta Talbiyah.”

na Hadiyth ya ´Aaishah:

“Watu watafufuliwa siku ya Qiyaamah wakiwa peku, uchi na bila kutahiriwa.”?

Jibu: Muhrim ni mwenye kuvuliwa kutoka katika hao. Yeye atafufuliwa siku ya Qiyaamah akiwa ni mwenye kuleta Talbiyah. Hakuna mgongano kati ya kwamba atafufuliwa siku ya Qiyaamah akiwa  peku, uchi na bila kutahiriwa na huku akileta Talbiyah. Kwa msemo mwingine yeye atawazidi kwa kule kuleta kwake Talbiyah. Lakini atakuwa kama wengine peku, uchi na bila kutahiriwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 15/08/2021