Swali: Ni ipi hukumu Muhrim akifunika mwili wake mzima kukiwemo kichwa wakati anapolala?

Jibu: Ajifunue. Akisahau, ajifunue na wala hakuna neno. Kadhalika kama alikuwa mjinga na akatambua hukumu kwamba haijuzu kufunika kichwa; ajifunue na wala hakuna kitu. Anapewa udhuru kwa kusahau na kwa ujinga. Na kama amelazimika kufunika kichwa chake kwa sababu ya baridi, basi afanye hivo na atalazimika kutoa fidia. Ni kama kunyoa wakati wa haja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (21) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 29/02/2020