Swali: Kuna mtu ana kiwango fulani cha pesa kwenye akaunti yake katika nchi yake. Pesa hii imeshapitikiwa na mwaka mmoja. Je, atoe zakaah huku au awakilishe mtu ambaye anaweza kumtolea katika nchi yake?

Jibu: Yote mawili yanajuzu. Akiwapa wale mafukara hapa, ndio bora zaidi. Akiwakilisha mtu ambaye atawapa mafukara katika nchi yake pia hakuna neno kufanya hivo. Jambo muhimu ni kwamba iwafikie mafukara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (79) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-11-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 02/11/2018