Muhammad Alizungumza Na Allaah?


Swali: Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizungumza na Mola Wake?

Jibu: Mola Wake alizungumza naye usiku safari ya mbinguni. Hata hivyo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumuona. Ama kuhusu Muusa (´alayhis-Salaam), Allaah Alizungumza naye. Ni mwenye kutofautiana na Mitume wengine kwa hili:

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

“Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno.” (04:164)

Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) ndiye mtu aliyezungumza na Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf--02041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2015