Muhammad al-Madkhaliy kuhusu maneno ya al-Qadhaafiy juu ya maandamano


Kuna kitu… Mtu huyu ambaye tutayataja maneno yake… Ninakuombeni udhuru kwa hili. Yanapatikana katika gazeti la al-Madiynah sehemu ya ar-Risaalah. Mimi ninaapa kwa Allaah ya kwamba sipendi kufanya hivi… Allaah ndiye anajau… Lakini nimelazimika… Huenda ndio mwanzo na mwisho… Siku ya Ijumaa al-Madiynah kulikuwa makala mbaya kabisa. Iko chini ya kichwa cha khabari: “Fatwa za wanachuoni ambazo zimetumiwa na serikali ya al-Qadhaafiy.” Yameandikwa na Dr. ´Aa´idh al-Qarniy. Ninacholenga ni maneno yake juu ya wanachuoni wenye kufuata Sunnah na Tawhiyd. Ameita katika maandamano na kutumia kama mfano wa maandamano ya Misri yaliyokuwepo wiki mbili zilizopita. Niliyasoma kwenye gazeti hili hili, lakini sijui kama yako al-Madiynah au kwenginepo. Nukta muhimu ni kwamba anazungumzia juu ya Mashaykh na wanachuoni wa Sunnah. Anasema: “Serikali ya Libya imewatumia wananchi wa Libya baadhi ya fatwa za wanachuoni zinazoharamisha kufanya uasi kwa watawala na kwamba maandamano ni haramu… ” (Tazama: http://www.al-madina.com/node/291389/risala) Hili si sahihi. Wanachuoni hawakusema hivi. Huu ni uongo. Pindi wanachuoni wanawapowazungumzisha ndugu zetu wa Libya, wanafanya hivo kwa ajili ya kulinda maisha yao. Hawakupatapo kusema haya juu ya al-Qadhaafiy. Anawasemea uongo. Kama jinsi alivyosema uongo al-Qadhaafiy, kadhalika amesema uongo ´Aa´idh. Hakuna tofauti kati yao inapokuja katika kuwasemea uongo wanachuoni. Wako sawa sawa. Huyu anasema uongo kwa ajili ya maslahi yake na yule mwengine, yaani ´Aa´idh al-Qarniy, anasema uongo kwa ajili ya maslahi ya madhehebu yake. Anafanya hivo ili kutaka kuwatukana wanachuoni. Dalili ya hilo ni pale ambapo baadhi waliwaashiria, walilibainisha suala hili na kwamba hawakuzungumza juu ya mtu huyu. Badala yake walizungumzia juu ya wananchi wa Libya kwa ajili ya kuokoa maisha yao. Haya hata na sisi tuliyabainisha hapo kabla. Kisha anasema: “Je, al-Qadhafiy ni mtawala ambaye ni wajibu kumtii na ni haramu kufanya uasi dhidi yake? Kadhalika inahusiana na kadhaa na kadhaa… ” Sikiliza: “Hawakuiungua Shari´ah ya Kiislamu? Hawakuwadhulumu wananchi? Hawakupora uhuru? Hawakufungua vituo? Hawakuwatesa waja wa Allaah? Hawakuziba vinywa? Hawakupora kipato cha serikali?” Kinachotuhusu hapa ni suala kuhusiana na Shari´ah na ndio ambalo tutalizungumza na wewe. Lau hili lisingekuwepo na kukawepo haya mengine yote, kuchukua mali, kuziba vinywa na mengineyo, haya yote isingelikuwa ni sababu ya kujuzu kufanya uasi kwake. Hatuzugumzi na wewe juu ya hili. Mahitajio ya pesa na uhuru na maneno mengine juu ya mateso ndio tamaa na lengo la al-Ikhwaan al-Muslimuun – na ´Aa´idh ni mmoja wao, sawa akipenda hilo au asilipende. Kinachozingatiwa ni matendo na maneno. Vinginevyo kila mmoja anaweza kudai ya kudai. Sikiliza anavyosema: “Ziko wapi fatwa za wanachuoni juu ya mambo kama haya ya khatari?” Bi maana kuhusu mali, kunyimwa uhuru wa kuzungumza, mateso, pato na mengineyo. Maneno ya wanachuoni juu ya mambo haya ni maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yanapatikana na yameandikwa kabla ya yeye kuumbwa, nayo ni kuwavumilia hata kama watakuchapa mgongo wako na kuchukua mali yako ambayo uliitokea jasho. Mtu asemeje sasa pale ambapo hawachukua mali yako wewe binafsi? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Sikiliza na tii hata kama watakupiga mgongo wako na kuchukua mali yako.” Tunacholenga si hichi. Wanachuoni hawakuzungumza kwa sura hii, ambayo ´Aa´idh anaijenga. Nukta hii hapa ninayoikusudia: “Ni wapi wamepata dalili ya kwamba maandamano ya amani ni haramu?” Haya ndio anayotaka kufikia: “Ni wapi wamepata dalili ya kwamba maandamano ya amani ni haramu? Ziko wapi dalili? Ni kwa nini kunatolea fatwa kama hizi za kuchagua ambazo zinatumiwa na kiongozi dhalimu na mkandamizaji wakati wa haja? Ni kwa nini wanasimama na fatwa zao pamoja na madikteta dhidi ya waathirikaji?” Kusema kwamba wanasimama na madikteta dhidi ya waathirikaji ni kuwasemea uongo. Kuhusiana na kwamba wanasimama pamoja na mtawala wa waislamu na anaamrisha yale yaliyoamrishwa na kiumbe bora (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ni kweli kwamba wanasema hivo pasi na kuona upungufu wowote, hata kama hilo halitokuridhisha. Haya ni maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maadamu mtawala ni muislamu, haya ni maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusiana na uharamu wa maandamano, mimi nakuuliza wewe una dalili gani juu ya maandamano? Hauna dalili yoyote zaidi ya kujifananisha na makafiri wa magharibi na mashariki. Anaonelea kuwa maandamano ya leo yanajuzu na anaita kuwa ni “maandamano ya amani” na anauliza dalili juu ya uharamu wake. Anaendelea kusema: “Wakati wananchi wenye kunyanyaswa na wenye kudhulumiwa na wasiokuwa na nguvu walipoanza kutoka nje katika maandamano ya amani kuandamana dhidi ya serikali hizi, ndipo wakaanza baadhi ya wanachuoni wetu kutoa fatwa zenye kuharamisha maandamano. Huu ni uelewa gani? Haya ni maarifa gani juu ya malengo ya Shari´ah? Uko wapi uelewa juu ya manufaa na madhara?” Haya ni katika maneno machafu na ya khatari kabisa. Hili si jambo la kushangaza kuona limetoka kwake na kutoka kwa watu mfano wake. Hakuna fitina yoyote isipikuwa yeye na watu mfano wake wako nyuma yake. Hakuna fitina yoyote isipokuwa wamo humo. Hakuna fitina yoyote isipokuwa wameshikamana nayo. Mashaykh na wanachuoni wa Sunnah ni wenye kuzungumza haki na kwa uadilifu pasi na kuangalia yako juu ya maslahi yao au dhidi yao. Haitakikani kupingana nao na kujenga picha ya kwamba ni wasaidizi wa madhalimu na wanyanyasaji. Hii ni jarima dhidi ya wanaume wenye kuibeba Shari´ah. Wenye kusema kuwa maandamano ni haramu ni wajuzi zaidi juu ya Shari´ah na dini ya Allaah na manufaa na madhara kuliko mtu huyu na watu mfano wake. Nimezungumza haya, jambo ambalo nimelizungumza pia katika matukio mbali mbali niliyoyatembelea, kwa sababu wasiokuwa wasomi wengi wanaweza kudanganyika kwa mara nyingine na mtu kama huyu na watu mfano wake kama Salmaan al-´Awdah na watu mfano wake. Ni wenye kuzunguka. Wamehadaika nao na kudhihiri kwao kwenye Televisheni za rasmi, chaneli za TV au karibu na baadhi ya viongozi. Wanasema kuwa wametubu kwa yale waliyoyasema katika vita vya Ghuba pindi Iraaq ilipovamia Kuwait. Msimamo wao na kashfa zao chafu zinajulikana. Kwa masikitiko makubwa wengi wanasahau. ´Awwaam hawaelewi kitu. Wanasema neno leo na kesho wanalisahau. Kwa masikitiko makubwa watu hawa wanalingania katika madhehebu. Lau wangelikuweko Misri basi wao ndio wangelikuwa wa kwanza kufanya uasi. Wangefanya vivyo hivyo katika miji mingine yote ambapo kunafanywa maandamano, hata kama mtawala angelikuwa muislamu. Wanafanya hivo kwa sababu amechukua mali na kusitisha uhuru wa kuzungumza. Hata hapa wangelikuwa wa kwanza kufanya uasi. Haya ndio wanayosema hivi sasa. Wanayasifu maandamano haya ya amani. Wanachuoni wa sasa vigogo wamesema kuwa maandamano haya ni haramu. Leo hii wana ngazi zile zile kama ambazo walizokuwa nazo wale maimamu wa hapo mwanzoni katika wakati wao. Maneno yao ni yenye kutosheleza. Ni waaminifu na maneno yao ni hoja. Shaykh al-Albaaniy. Shaykh na Imaam Ibn Baaz. Shaykh Ibn ´Uthaymiyn. Shaykh al-Fawzaan. al-Lajnah ad-Daaimah katika kipindi kile. Ilikuwa zamani sana. Kadhalika wanachuoni wengine wa Sunnah wamesema katika sehemu zote. Wana fataawaa za wazi kuhusiana na mada hii na kwamba maandamano ni haramu na kwamba yamekuja kutoka kwa makafiri wa mashariki au magharibi na khaswa Ulaya na Marekani. Dalili kubwa yenye kuonesha kuwa wanachuoni wetu wanazungumza kweli – na wanazungumza kweli na wala hawana haja ya sisi kuwasadikisha – ni kwamba magharibi, Ulaya na Marekani ndio wenye kuita katika kuwapa wananchi haki zao za maandamano ya amani. Wao ndio walioko nyuma ya fitina hizi. Hivi sasa ´Aa´idh al-Qarniy, Salmaan na wengineo wanaiweka mikono yao nyuma ya mkono wa magharibi dhidi ya watawala wa Kiislamu. Hivi sasa asijitokeze mtu na kunisemea uongo ya kwamba Muhammad bin Haadiy amesema hili na lile juu ya huyu na yule. Mimi nazungumzia mtawala wa Kiislamu. Maadamu ni muislamu vovyote atavyofanya midhali hajatoka katika Uislamu haijuzu kumfanyia uasi. Kuhusiana na kafiri, hatumzungumzi yeye. Mimi tangu miaka thelathini ya nyuma naonelea kuwa al-Qadhaafiy ni kafiri. Niliwaambia haya watoto wetu wa Libya tangu hapo kabla. Lakini kama jinsi al-Qadhaafiy anatumia maneno haya, ´Aa´idh al-Qarniy anafanya hayo kwa njia mbaya zaidi. Kwa sababu anajua kuwa hawa hawasemi aliyoyajengea picha. Lakini Allaah ni mwenye kutotosheleza na yeye ndiye mbora wa kuyaangalia mambo.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=119354
  • Imechapishwa: 04/05/2018