Muhammad al-Madkhaliy anawatukana Ahl-us-Sunnah?


Swali: Ni yepi maoni yako kwa yule mwenye kusema kuwa Shaykh Muhammad bin Haadiy anawatukana na kuwatahadharisha Ahl-us-Sunnah?

Jibu: Bali Shaykh Muhammad bin Haadiy (Hafidhwahu Allaah) anawatukana Ahl-ul-Bid´ah na wapotevu kwa ajili ya kuutakia Uislamu na waislamu kheri na vilevile kwa ajili ya kuitakasa dhimmah. Iwapo si fadhila ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) juu ya Uislamu na waislamu kwa mfano wa wanachuoni kama hawa basi haki isingeliwabainikia watu. Vilevile wasingelijua njia ya uongofu na wala wasingejiepusha na njia ya upotevu. Ni wanachuoni kama mfano wa Shaykh Rabiy´, Shaykh ´Ubayd, Shaykh Muhammad bin Haadiy na mfano wao, ndugu zao na wanafunzi wao ambao wanasimamia kazi hii.  Wanawatakia watu kheri. Mfano wa matendo kama haya yanatakiwa kutajwa na kushukuriwa. Yeye, ndugu zake, waalimu zake na wanafunzi wake wanatakiwa kusapotiwa kwa yale wanayoyafanya na kupita juu ya njia hii.

Mimi namuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amruzuku Shaykh Muhammad bin Haadiy na wanachuoni wakubwa wa Ahl-us-Sunnah kama mfano wa Shaykh Rabiy´ na Shaykh Swaalih al-Fawzaan, awatunuku uimara, mwisho mwema, siha na afya, na awafanye Ahl-ul-Bid´ah na wapotevu wayaone maisha machungu, aunusuru Uislamu na waislamu kupitia wao na awajaze kheri kikwelikweli kwa vile wanavowatakia waislamu kheri, kuutetea Uislamu na waislamu kheri na kuwafichua na kuwafedhehesha Ahl-ul-Bid´ah na kutahadharisha nao.

Ninamuomba Allaah atusaidie sisi na wao, mafanikio, uongofu, ukomavu na umakini.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin ´Umar Baazmuul
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ia902609.us.archive.org/29/items/mohammad-bazmool/mohammad-bazmool.mp3
  • Imechapishwa: 04/11/2017