Hakika Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametubainishia njia moja ambayo ni lazima kwa waislamu kuifuata. Nayo si nyingine ni njia ya Allaah iliyonyooka na mfumo imara wa dini Yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Kwamba hii ni njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate njia za vichochoro nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo alivyokuusieni kwayo mpate kumcha.”[1]

Kwa hivyo ni wajibu kwa wanachuoni waislamu kuweka wazi uhakika wa mambo na kujadili na kila kundi. Nawanasihi wote kupita juu ya msitari ambao Allaah amewachorea waja Wake na Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akalingania kwayo. Mwenye kuivuka au akaendelea juu ya ukaidi wake basi lililo la wajibu ni kumfedhehi na kumtahadharisha kwa yule anayejua uhakika wa mambo ili watu wajiepushe na mfumo wake na ili wasimfuate wale wasiojua uhakika wa jambo lake hatimaye akampoteza na akamtoa nje ya njia ilionyooka ambayo Allaah katuamrisha kuifuata… Hapana shaka kwamba mapote na makundi mengi katika mji wa waislamu shaytwaan anayapupia kwanza na baada ya hapo maadui wa Uislamu katika wanadamu.

[1] 06:153

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 406
  • Imechapishwa: 08/03/2020