Muda wa kukata swawm kwa abiria ndani ya ndege

Swali: Ni upi muda wa kukata swawm kwa aliye ndani ya ndege katika Ramadhaan?

Jibu: Mtu akiwa ndani ya ndege mchana wa Ramadhaan na akapenda kuendelea na swawm yake mpaka usiku, basi haijuzu kwake kukata swawm isipokuwa baada ya kuzama kwa jua kwa mujibu wa abiria.

  • Mhusika: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/138)
  • Imechapishwa: 30/05/2017